Mbinu mbili (2) zitakazokusaidia kufanikiwa katika biashara
Upo usemi mmoja hivi mzuri unaosema " Rome was not built in a day" Kwa kibantu ni kwamba Roma haikujengwa kwa siku moja. Ndugu unapotaka mafanikio katika biashara siyo kwamba mafanikio hayo utayapata ndani ya siku moja la hasha kitu kama hicho hakipo hata utambike.
Ukweli ni kwamba ukuaji wa biashara na mafanikio yaliyonona ndani yake hutokana na uimara wa mtu huyo kujifunza mbinu mbalimbali za msingi zitakazomsaidia mfanyabiashara huyo aweze kufanikiwa katika biashara anayoifanya.
Siku ya leo nitakueleza japo kwa uchache mbinu muhimu zitakazokusaidia kuweza kufanikiwa katika biashara unayoifanya kama ifutaavyo;
Ifahamike kuwa ili uweze kufanikiwa katika biashara unayoifanya au unayoitaka kuifanya ni kwamba ni lazima uweze kuwa mbunifu, kila wakati angalia mbele kwa kutambua mbinu zitakazokusaidia kuweza kuikuza biashara yako. Ili uweze kuwa mbunifu katika biashara yako akili yako ijikite zaidi katika kuwaza mawazo mapya na njia mpya za kufanya biashara.
Kama utawekeza mawazo yako katika kusimamia mawazo yako ya kale ni kwamba kila siku utapata matokeo yale yale kila wakati, hivyo kila wakati ni lazima uelewe ili uweze kukua katika biashara basi mawazo chanya na yenye ubunifu ndani yake ni muhimu kuyazingatia ili kuikuza biashara.
Kitu kingine ambacho kitakusaidia kufanikiwa katika biashara yako ni kuwa makini na mahesabu yako ya kibiashara, Mtaji ufahamike na faida ifahamike pia. Katika hili unatakiwa kuzingatia kitu kinachoitwa mapato na matumizi.
Usipokuwa na makini na mahesabu yako ni kwamba hatukuwa na maisha marefu katika biashara yako, hivyo kila wakati unatakiwa kujifunza mbinu maridhawa za kufanya mahesabu yako ili kujua kama unapata faida ama laah, jambo hili ni muhimu sana kwa sababu ni chachu ya msingi katika kuongeza thawabu kubwa katika biashara yako.
Pia unashauriwa ya kwamba unatakiwa kupangilia kazi katika biashara yako.
Kila siku ushinde katika biashara yako pasipo kuwa na jukumu ambalo umelipanga kulifanya, unatakiwa kabla ya kutoka nyumbani kwako lazima uwe na ratiba ambayo inahusiana na mambo ambayo utayafanya kwa siku husika.
Kama ni kupiga hesabu, kuwaza mbinu mpya za ubunifu wa kibiashara, kufanya usafi, na mambo mengine kama hayo yatakayoifanya biashara yako ikue zaidi basi ni mambo ambayo unapaswa kuyapangilia kuyafanya kwa siku husika katika kazi zako.

Ukiyazingatia haya kwa ukaribu na kwa umakini basi mafanikio makubwa yatakuwa upande wako katika biashara unayoifanya.

Comments
Post a Comment