Mipango ya kuifahamu kabla ya kuanzisha biashara
MipaMalengo ni lazima yaende sambamba na mipango ili kuweza kutimiza ndoto zako kibiashara, hata hivyo huenda ukawa haujanielewa, ipo hivi, mipango ni mtiriko wa namna ya kuyafikia malengo. Pia malengo ni lazima yaanze katika ngazi ya chini kabisa, hapa nikiwa na maana ni lazima uanze na malengo madogo madogo au watalaamu wa masuala ya mafanikio huita (baby step). Malengo ya kibiashara ni njia sahihi ya kufanikiwa kwako kibiashara, kuna baadhi ya watu wao hufanya mambo ambayo hayana mipango na mikakati ambayo itawasababisha kuweza kutimiza ndoto zao ambazo wamejipangia katika masuala mazima ya kibiashara. Na kufanya hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, kwani kila siku utajiona ni mnyonge, huna faida za kuendelea kuishi, hufai hii ni kutoka na kutoiona faida yeyote katika biashara ambayo unaifanya. Yafutayo ni maswali muhimu ambayo ni muhimu kujiuliza katika upangaji wa malengo ya uanzishaji kibiashara; 1. Eneo kwa ajili ya kufanyia biashara. Ku...