Posts

Showing posts from July, 2020

Mambo ya kuzingatia pale unapoanzisha Biashara

Image
Njia pekee itakuyokusaidia kuingiza kipato cha ziada na kukupeleka kwenye uhuru wa kifedha ni kwa wewe kuamua kuanzisha biashara yako na utakayoamua kuisimamia kikamilifu hadi ikuletee mafanikio. Ili kuanzisha biashara na ikafika mahali ukaanza kuona matunda ya biashara yako, kwa kawaida huwa ipo misingi au mambo ambayo unatakiwa uzingatie sana ili biashara yako iweze kudumu na kutoa faida uitakayo. Yafuatayo Ni Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.  1. Elewa wateja wako wa mwanzo wanataka nini na hapo utapata picha ya jinsi utavyoiendesha biashara na uzingativu juu ya kazi. Ukijua wateja wako wanataka kitu gani, itakusaidia sana kuweza kuwapa huduma hiyo. 2. Kuwa mbunifu,  hilo ndilo jambo kubwa zaidi, biashara ni zilezile ila kinachofanya wateja wakimbilie biashara  yako ni ubunifu wako. Kama usipokuwa mbunifu na ukataka kufanikiwa kibiashara uwe na uhakika utakwama. 3. Lugha nzuri kwa wateja na ukarimu, huweza kumasisha kuongezeka wa wateja wengi kati...

Wekeza katika jambo hili utafanikiwa

Image
Fanya Uwekezaji kwa Wale Uwapendao/Ndugu/Marafiki na Jamii. Huu ni uwekezaji kwa wale unaowapenda na kwa jamii inayokuzunguka. Hapa kwa wewe ambaye una mke/mume/Watoto/ndugu na marafiki utapaswa kufanya kitu kwa ajili yao. Vile vile utapaswa kufanya kitu kwenye jamii inayokuzunguka. Sio lazima ukifanyacho kiwe ni kinahitaji fedha bali kiwe ni kitu chenye kuongeza thamani na kinachogusa Maisha yao. (Jamii inaweza Kuwa Mtaa Unaoishi/ulikotoka, kanisani/msikitini unakosali.). Kwa kupitia kuwekeza kwa hawa watu miaka ijayo utakuja kuyaona matunda ya uwekezaji wako. Utazungukwa na jamii ambayo inatokana na uwekezaji wako kwao. Utaishi Maisha ya furaha kwasababu uliweza kuitengeneza jamii ambayo ulikuwa unaitaka. Mke/mume/Watoto hawawezi kuwa vile unavyotaka kama wewe hujachangia. Badilisha kile unachowekeza kwao kila siku. Maneno yako unayoongea nao ni uwekezaji, vile unavyowatendea ni uwekezaji miaka michache ijayo watakuwa kile ulichokuwa unawafanyia. Sasa jiulize wewe umepambana ...

Kama unataka kuwa Mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, Acha kufanya mambo haya

Image
Mara nyingi huwa sio kitu kigeni kwa mtu ambaye ni  mjasiriamli wakati mwingine kufanya maamuzi yasiyo sahihi, kukosea hapa na pale na hata wakati mwingine kufanya biashara na watu ambao sio sahihi ambao wanauwezo wa kukurudisha nyuma, hii huwa inatokea sana bila kujua. Hiyo yote inakuja kutuonyesha kuwa katika suala zima la ujasiriamali makosa huwa yapo na ni muhimu sana kuweza kutusaidia kusonga mbele pale tunapochukua jukumu la kujifunza kutokana na makosa. Hata hivyo huwa yapo makosa ambayo huwa tunaweza kuyaepuka ikiwa kweli tuna nia ya kuwa wajasiriamali wakubwa. Kama unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, acha kufanya mambo haya:- 1. Acha kuogopa sana ushindani wa kibiashara. Ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, kitu pekee ambacho hutakiwi kuogopa sana ni ushindani wa kibiashara. Badala ya kuogopa ushindani kaa chini na kisha ujifunze ni kitu gani unachotakiwa ufanye katikati ya ushindani huo mkubwa unaouona. Kama una jiamini na bidhaa zako sok...

Zifahamu aina 9 za wateja ili ukuze Biashara yako

Image
Mteja ni nani? Mteja ni mtu yeyote anayenunua bidhaa au huduma inayotolewa na biashara fulani. Mteja ni mtu muhimu sana katika biashara yoyote. Lengo la kuanzisha biashara ni kupata wateja watakaonunua bidhaa au  huduma yako. Biashara yoyote isipopata wateja bora na wa uhakika, ni wazi kuwa haiwezi kufanikiwa; itakufa tu. Kutokana na kukosa uelewa, wafanyabiashara wengi hawawafahamu wateja vyema, hivyo kutokuwamudu vyema; jambo ambalo huwakwamisha kufikia malengo yao. Ikiwa wewe ni mfanya biashara tayari au unataka kuanza kufanya biashara, karibu nikushirikishe aina 9 za wateja unazoweza kuzitumia kukuza biashara yako. 1. Wateja wapya Hawa ni wateja ambao huja kwenye biashara yako kwa mara ya kwanza, mnaweza kuwa mnafahamiana nje ya biashara, lakini hamjawahi kuhudumiana kwenye biashara. Mteja huyu huja kwa lengo la kupata huduma pamoja na  kuifahamu biashara husika ili kuona sababu itakayomfanya awe mteja wa biashara hiyo. Wewe kama mfanyabiashara, hutakiwi kufanya ko...

Mambo 5 yanayosababisha Biashara nyingi za Wanawake kufa

Image
Hivi leo wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahi na kufanyia kazi fursa mbalimbali. Fursa hizo ni pamoja na uwekezaji katika biashara ndogo na za kati. Ni dhahiri kuwa mama ndiye nayeumia zaidi pale familia inapokuwa na uchumi mbaya. Mama hapendi kuona watoto wanakosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu, matibabu n.k. Hivyo suala la kuboresha kipato cha familia limewafanya wanawake wengi kutafuta njia mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo njia ya kufanya biashara. Hata hivyo pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na wanawake, bado biashara zao ngingi hufa kutokana na sababu kadha wa kadha. Fuatana nami katika makala hii ufahamu mambo matano yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa. 1. Kukosa maarifa na elimu ya biashara Kitu chochote au kazi yoyote inahitaji maarifa stahiki ili uweze kuifanya kwa kwa ufanisi. Ni dhahiri kuwa wanawake wengi huanzisha biashara pasipo kujiandaa kimaarifa au kutafuta ujuzi unaohitajika katika kuendesha biashara hu...

Namna ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo

Image
Watu wengi wamekuwa wakitamani kuanza biashara lakini wanafikiri namna ya kuanza kwani mtaji wao ni mdogo sana. Usiogope; kuwa na mtaji mdogo au kutokuwa nao kabisa sio mwisho wako wa kutimiza malengo yako. “Usilie juu ya kile ambacho huna; tumia vizuri kile ulichonacho.” - Reginald Mengi Zipo mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kukuwezesha kufanya biashara hata kama utakuwa na mtaji mdogo. Tafadhali fuatilia hoja jadiliwa hapo chini kwa ufafanuzi zaidi. 1. Kuwa mbunifu Moja kati ya mambo ambayo yatakusaidia sana kwenye kuanza biashara kwa mtaji mdogo ni ubunifu. Kwa njia ya ubunifu utaweza kushinda biashara na bidhaa zilizoko sokoni kwa urahisi zaidi. Unaweza kufanya haya yafuatayo: Chagua wazo la biashara unalolipenda na kuliweza vyema. Hili litakusaidia kukabili changamoto vyema. Angalia tatizo au uhitaji uliopo sasa na uutatue kwa bidhaa au huduma yako. Panga bei vizuri; unaweza kuweka bei ambayo ni tofauti kidogo na bidhaa au huduma ambazo tayari ziko sokoni ili uwavutie wate...

Zijue sifa 10 ambazo kila Mjasiriamali anatakiwa kuwa nazo

Image
Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujipatia kipato. Hivi leo kuna wajasiriamali wengi waliofanikiwa na wengine hawajafanikiwa. Kwa hakika wajasiriamali waliofanikiwa wanafahamu na wanaziishi sifa za wajasiriamali bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa mjasiriamali bora wakati una sifa za mwajiriwa. Ili kuwa mjasiriamali ni lazima kuzifahamu na kuziishi sifa za mjasiriamali. Karibu nikufahamishe sifa 10 za mjasiriamali. 1. Mwenye malengo Malengo ni mwongozo wa kukuwezesha kufanikisha jambo lolote. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Je umeamua kuwa mjasiriamali kwenye nini? Kwa ajili ya nini? Malengo yatakuongoza ufanye nini, wapi lini na kwa ajili ya nini. Bila malengo utafanya mambo bila mwongozo wowote na ni vigumu kufanikiwa. 2. Nidhamu Nidhamu ni sifa muhimu kwa mjasiriamali kwani itamtenga na mambo mengi yasiyokuwa na umuhimu. Ni lazima mjasiriamali awe na nidhamu ya maswala kama vile matumizi ya muda...