Posts

Mipango ya kuifahamu kabla ya kuanzisha biashara

Image
  MipaMalengo ni lazima yaende sambamba na mipango ili kuweza kutimiza ndoto zako kibiashara, hata hivyo huenda ukawa haujanielewa, ipo hivi, mipango ni mtiriko wa namna ya kuyafikia malengo. Pia malengo ni lazima yaanze katika ngazi ya chini kabisa, hapa nikiwa na maana ni lazima uanze na malengo madogo madogo au watalaamu wa masuala ya mafanikio huita (baby step). Malengo ya kibiashara ni njia sahihi ya kufanikiwa kwako kibiashara, kuna baadhi ya watu wao hufanya mambo ambayo hayana mipango na mikakati ambayo itawasababisha kuweza kutimiza ndoto zao ambazo wamejipangia katika masuala mazima ya kibiashara. Na kufanya hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, kwani kila siku utajiona ni mnyonge, huna faida za kuendelea kuishi, hufai hii ni kutoka na kutoiona faida yeyote katika biashara ambayo unaifanya. Yafutayo ni maswali muhimu ambayo ni muhimu kujiuliza  katika upangaji wa malengo ya uanzishaji kibiashara; 1. Eneo kwa ajili ya kufanyia biashara. Ku...

Zijue aina za biashara unazoweza kuzifanya pasipo na mtaji

Image
  Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndio uanzishe biashara na ndio sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha, Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu sana katika kuanzisha biashara, lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo sana kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa sana. Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana  kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services) na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako, kuajiri watu wengine nk , ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi fulani hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na degree ya chuo kikuu. Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali, workshop mbalimbali, au kufundishwa na mtu wenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuan...

Mambo 6 ambayo Mjasiriamali anatakiwa kuyafanya kila siku

Image
  Kati ya kitu ambacho kila mjasiriamali mwenye nia ya kufanikiwa anacho ni kule kutaka kuona anakifikia mafanikio makubwa ya kibiashara. Lakini pamoja na kuwa na nia hiyo ya kufikia mafanikio hayo, mjasiriamali huyu hawezi kufanikiwa mpaka ajue mambo ya msingi yanayoweza kumsaidia kufanikiwa na kuyafanya karibu kila siku. Kwa mjasiriamali yoyote atakayeelewa mambo hayo itamsaidia sana kuweza kufikia mafanikio makubwa anayohitaji. Kwa kujifunza kupitia makala haya, itakuonyesha mambo ya wazi ambayo unatakiwa kuyajua kama mjasiriamali na kuyafanya kila wakati ili kuweza kufanikiwa. Sasa twende pamoja kuweza kujifunza mambo unayotakiwa kuyazingatia kila siku katika safari yako ya mafanikio. 1. Panga siku yako mapema. Ni rahisi sana siku yako kuwa ya mafanikio ikiwa utaipangilia mapema. Ni vizuri ukaipangilia siku yako mapema ikiwezekana siku moja kabla ili kuweza kujua ni kitu gani utakachokifanya kesho. Hiyo itakusaidia kuweka malengo na kupanga mikakati muhimu...

Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuomba mkopo

Image
  Kutokana na kipato cha watu wengi kutokutosheleza mahitaji yao, hujikuta wakilazimika kukopa. Wapo waliofanikiwa sana kwenye mipango yao kutokana na mikopo, lakini wapo pia waliofilisika kutokana na mikopo. Kwa hakika swala la mikopo linahitaji umakini mkubwa pamoja na mipango na mikakati stahiki ili lisije likakuingiza kwenye madeni yasiyokwisha. Ikiwa una mpango wa kukopa, basi fahamu mambo matano muhimu ya kuzingatia kabla ya kuomba mkopo. 1. Bainisha uwezo wako wa kifedha Ili upate na utumie mkopo vyema, ni muhimu ufahamu uwezo wako wa kifedha. Ikiwa uwezo wako wa kifedha ni shilingi milioni moja, ukikopa mkopo wa bilioni 1 hutoweza kuupata wala kuurejesha. Hakikisha unatathimini kipato chako pamoja na uwezo wako wa kutumia pesa ili usije ukatumbukia kwenye madeni. 2. Andaa mpango wa matumizi na marejesho Watu wengi hushindwa kupata mkopo au kurejesha mkopo kutokana na kutokuwa na mpango mzuri wa matumizi na urejeshaji wa mkopo. Hakikisha kabla ya kukopa ...

Zitambue athari 5 za kukopesha Pesa na Bidhaa kwa Wateja

Image
  Katika jaamii zetu za kiafrika suala la mikopo ya bidhaa au fedha kutoka kwenye biashara kwenda kwa wateja limezoeleka sana. Ingawa jambo hili linaweza kuwa na manufaa kwa upande fulani, hata hivyo kutokana na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu wengi jambo hili limekuwa na athari nyingi kuliko faida. Inawezekana umekuwa ukiwakopesha wateja wako wa maana sana, au umekuwa ukitumia mikopo kama njia ya kuuza huduma au bidhaa zako, lakini karibu nikushirikishe athari tano za mikopo hiyo. 1. Kumpoteza mteja Kuna usemi usemao kumkopesha mteja ni kumfukuza. Nimesikia mara kadhaa wafanyabiashara wakisema tangu ni mkopeshe haji tena dukani kwangu, au tangu nimkopeshe anapita mbali tu. Mara nyingi mteja akishakopeshwa pesa au bidhaa haji tena kwenye biashara husika ili kukwepa kulipa deni.  Kuliko umpoteze mteja kwa kumkopesha ni bora umueleze ukweli kwa kutumia busara; ingawa hatofurahi kwa wakati ule lakini baada ya muda atakuelewa na ataendelea kuwa mteja wako....

Tofauti 10 kati ya Mwajiriwa na Mjasiriamali

Image
  Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya mwajiriwa na mjasriamali; tofauti hii inahusisha tabia, fikra, maamuzi au hata matendo. Kuna baadhi ya watu ni wajasiriamali kwa mwonekano lakini kitabia ni waajiriwa; wapo pia wengine ni waajiriwa kimwonekano lakini ni wajasiriamali kitabia. Ikiwa basi unataka kuwa mjasiriamali, ni muhimu ufahamu tofauti 10 za msingi zilizopo kati ya mwajiriwa na mjasiriamali. 1. Mwajiriwa hupumzika kwenye likizo lakini mjasiriamali hutumia likizo kufanya kazi zaidi Kwa kawaida waajiriwa hufurahia muda wa likizo kwa sababu ndipo hupata muda wa kupumzika. Hali ni tofauti kwa mjasiriamali kwani hana likizo, na ikiwa ni mjasiriamali aliyeajiriwa, basi atatumia likizo yake kuendeleza mradi au biashara yake. 2. Mwajiriwa hulenga kupanda cheo lakini mjasiriamali hulenga kukuza mradi wake Mwajiriwa kila mara anafanya kazi kwa bidii ili apandishwe cheo au aongezewe mshahara na marupurupu. Mjasiriamali kila mara huwaza na kutekeleza mikakati mbalimbali ya kukuza au k...

Mbinu za kuongeza mauzo katika biashara

Image
  Kwanza kabisa ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara ambayo unaifanya unatakiwa kuachana na mfumo wa zamani ambao ulikuwa unatumia katika kufanya biashara yako, kama inashindikana kuachana na mfumo huo wa zamani basi unachotakiwa kufanya ni kuboresha mfumo huo wa zamani ili uweze kufanikiwa kibiashara. Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa kulikumbatia katika biashara yako ni,  kuelewa mbinu za kufanya biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii.  Kwa wenzetu wazungu mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia kutengeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani. Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi dunia ya...